Kocha wa Manchester United Jose Mourinho anazidi kutafuta wa
kumuangushia mzigo wa lawama kutokana timu hiyo kutofanya vizuri na
kusema kwamba, wachezaji wake wanashindwa kufuata maelekezo yake
kutokana na kuathiriwa na falsafa za kocha wao wa zamani Louis van Gaal.
Manchester United wamepoteza mechi tatu mfululizo, na mchezo wa leo wa
Kombe la EFL dhidi ya Northampton Town utakuwa muhimu katika kuhakikisha
wanafuta hasira za mashabiki wao.
Kwa takribani siku kumi Mourinho amekuwa akiwakosoa wachezaji wake
hadharani, hali ambayo imekosolewa vikali na wadau na wachambuzi
mbalimbali wa soka, wakieleza kuwa masuala hayo yalitakiwa kumalizwa
ndani kwa ndani.
Mwezi uliopita bosi huyo wa United aliweka wazi kuwa, angekuwa na wakati
mgumu sana kupandikiza falsafa zake kutokana na wachezaji wengi kuwa
bado na falsafa za mtangulizi wake Van Gaal ambaye alidumu klabuni hapo
kwa miaka miwili, akisema wachezaji hao walikuwa kama marobot.
‘Ni vigumu sana kubadilisha mfumo,’ alisema. ‘Ingekuwa rahisi zaidi
kwangu kuwa na wachezaji wapya 20 na nianze mwanzo kila kitu.
‘Kwa miaka miwili walikuwa na wakitumia mfumo ambao ni tofauti na wangu.’
Ander Herrera ni moja ya wachezaji waliotolewa mfano kwamba
wanachanganya namna ya uchezaji kati ya matumizi ya mfumo mpya wa
Mourinho au ule wa awali wa Van Gaal.
Mabeki wa pembeni pia wanahangaika kuendana na mfumo mpya. Mourinho
anawataka kupanda na kupeleka mashambulizi kwa kasi, wakati walikuwa
wakielekezwa tofauti chini ya utawala wa Van Gaal.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni