Katika mchakato huo, wizara hiyo itashirikiana na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), ambayo itaratibu mchakato wote wa utambuzi, kuhakiki taarifa za watumishi na kuchukua alama za vidole.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Angella Kairuki amesema mchakato huo utafanyika kwa wiki mbili kuanzia Oktoba 3 na utawahusisha watumishi wa wizara, taasisi za Serikali zinazojitegemea, tawala za mikoa, mamlaka za Serikali za Mitaa na mashirika ya umma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni