Wizara ya mambo ya ndani ya Marekani imesema kuwa Washington na Moscow wamekubaliana kusitisha mapigano saa nyingine 48. Usitishwaji huo uliondaliwa na nchi hizo mbili umeleta matokeo kwa siku mbili na waangalizi wanasema kuwa hakuna watu waliokufa ndani ya siku hizo licha ya kuwepo kwa vurugu kadhaa.
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa kukosekana kwa maandalizi ya kiusalama bado kuna kwamisha misaada ya kibinadamu.
Ameongeza kuwa aliiomba Moscow na Washington kushirikiana na washirika wao ili kuhakikisha misaada inafika kwa wakati.
Uondoaji wa vikosi vya waasi na serikali katika maeneo ya barabara muhimu unatarajiwa kuanza leo.
Umoja wa mataifa bado hawajaweza kupeleka misaada ya kutosha ya kibinadamu katika maeneo yaliyozingirwa huko Syria, hususani katika maeneo yanashikiliwa na waasi Mashariki mwa Aleppo licha ya kusitishwa kwa mapigano.
Magari ya Urusi yamefika maeneo yanayoshikiliwa na serikali huko jimbo la Homs.
Wanasiasa wapinzani wanasema kuwa serikali ya Syria ilisisitiza kusambaza na kusimamia misaada hali inayozuia usambazaji wake, lakini mwandishi wa BBC amesema kuwa haja ya kupata usalama kutoka kwa makundi ya waasi nayo inachingia ucheleweshaji huo.
Msafara wa magari ya misaada ya umoja wa mataifa unasubiri kupewa ruhusa ya kupita katika mpaka wa Uturuki kuingia Aleppo.
Carsten Hansen anatoka baraza la wakimbizi la Norway, wameweza kusambaza misaada katika baadhi ya meoneo nchini Syria.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni