Sergio Aguero amefunga 'hat-trick' yake ya pili msimu huu na kuwawezesha Manchester City kupata ushindi mnono dhidi ya Borussia Monchengladbach ya Ujerumani katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Baadaye alimchenga kipa na kufunga bao kwenye lango wazi dakika ya 77.
Mechi hiyo ilitazamwa na mashabiki 32,000, baada ya kuahirishwa kutoka Jumanne kutokana na mvua.
Nguvu mpya Kelechi Iheanacho alikamilisha ufungaji dakika za mwisho mwisho
Sergio Aguero, 28, sasa amefunga mabao 25 Ligi ya Mabingwa, moja zaidi ya nyota wa zamani wa Manchester United Paul Scholes.
Aguero atakosa mechi ya Jumamosi Ligi ya Premia dhidi ya Bournemouth na mechi ya Kombe la Ligi ugenini Swansea kutokana na marufuku ya mechi tatu anayoendelea kuitumikia.
City watarejea tena kucheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya tarehe 28 Septemba ugenini kwa Celtic, waliochapwa 7-0 na Barcelona Jumanne.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni