Dully Sykes anaamini kuwa ili msanii aweze kuwa ‘legend’ ni lazima apitie hatua ya kuandikiwa nyimbo.
Akiongea na Perfect katika 255 ya Clouds FM, Dully alisema kuwa wimbo wake ‘Inde’ amesaidiwa kuuandika na Raymond wa WCB.
“Inde nimesaidiwa kuandika na Raymond, nyimbo nyingine ambayo
nimeandikiwa ni dhahabu. Kwenye nyimbo hiyo chorus niliandika mwenyewe
ila verse nilisaidiwa na msanii anaitwa Jay C ambaye alishawahi kufanya
kazi na Q Chilla wimbo wa Mpiga Debe,” alisema Dully Sykes
“Hakuna legend ambaye hajawahi kuandikiwa na pia huwezi kuwa Legend kama
hujawahi kuandikiwa, kwasababu legend si mjivuni,” alisisitiza.
Hadi sasa Inde umekuwa wimbo wenye mafanikio makubwa kwa msanii huyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni