Zaidi ya $200,000 zimechangishwa kwenye mtandao wa kijamii kumsaidia mwanamme mmoja mkongwe, anayeuza aiskrimu katika jimbo la Chicago Marekani, baada ya kuonekana kwa picha aking'ang'ana kusukuma toroli iliyojaa aiskrimu!
Fidencio Sanchez, 89, alilazimika kustaafu majira ya kiangazi, baada ya bintiye kuaga dunia, na ikambidi awe mlezi wa wajukuu wake.
Ukurasa wa facebook, #GoFundMe, ulianzishwa na mtu asiyejulikana, aliyeguswa hisia zake baada ya kumwona mwanamme huyo mkongwe akiwa amejipinda kwenye toroli yake.
Hata baada ya mchango huo, bwana Sanchez anasema kwamba hatowachana na kazi hiyo.
Bwana Sanchez amekuwa akiuza aiskrimu mitaani kwa miaka 23.
Alikuwa amestaafu kwa miezi miwili pekee wakati binti yake alifariki mwezi Julai.
Bwana Sanchez, aliamua kurejea kazini ili kuwasaidia wajukuu wake na mkewe anayeugua kwa sasa.
Aliyeanzisha kampeni ya kuchangisha pesa mitandaoni alikuwa analenga kupata $3,000 , japo alipata pesa zaidi chini ya saa moja,
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni