Kibaha. Mkazi wa Kibaha, Michael William maarufu ‘Michael Dada’ ameuawa
kwa kupigwa na wananchi katika msitu wa Shirika la Elimu Kibaha kutokana
na tuhuma za kuteka watoto wawili wa kike kwa lengo la kuwabaka.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Boniveture Mushongi alisema jana kuwa mtuhumiwa huyo aliuawa Alhamisi saa 10:00 jioni.
Alisema Michael Dada anadaiwa kuwateka watoto hao ambao ni wanafunzi wa
darasa la nne wa Shule ya Msingi Kibaha na mwingine wa Shule ya Awali ya
Mama Kawili mchana wakati wanacheza jirani na nyumbani kwao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni