
Polisi katika jimbo la Washington nchini Marekani wamemkamata mshukiwa mmoja kuhusiana na kisa ambapo watu watano walipigwa risasi na kuuwawa katika jengo moja la kibiashara siku ya Ijumaa.
Wamemtaja mshukiwa huyo kwa jina Arcan Cetin mwenye umri wa miaka 20.
Kiini cha mauaji hayo yaliyotokea katika jumba la biashara kwenye mji wa Burlington bado hakijulikani. Aidha polisi wanasema kuwa mshukiwa huyo hana historia ya kuwa na uhusiano na makundi yenye siasa kali
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni