Hivi punde majira ya saa 9:27 asubuhi eneo la Legeza wilayani Newala
Barabara ya kuelekea mkoani Mtwara. imetokea ajali imehusisha gari aina
ya Subaru-impreza yenye namba ya usajili T684DHY iliyokuwa ikitokea
Newala mjini ndipo dereva alipofika katika kijiji hicho (legeza)
alishindwa kuimudu gari hiyo hatimaye kuvamia tuta lililokuwa pembezoni
mwa barabara kitendo kilichofanya gari hiyo kugeuka mara tatu.Hata hivyo
hakuna kifo kilichojitokeza isipokuwa watoto wawili na dereva ni
majeruhi,wote walikuwa kwenye gari hiyo na wamepelekwa hospitali ya
wilaya ya Newala kwa matibabu zaidi.
Picha za Ajali hiyo..
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni