Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa
Ilioishia
Nilimuuliza dorecy na kumfanya phidaya kunitazama kwa jicho kali lililo jaa hasira
“ndio, ila kuna ishu khalid alitaka kukufanyia wewe na phidaya akaiingilia kati na kuwa adui mwengine wa khalid”
“jambo gani hilo?”
Hata
kabla dorecy hajanijibu tukasikia milio mingi ya risasi kwenye kordo
yetu huku kelele za watu wagonjwa na manesi wakike zikisikia jambo
lililo tushtua sote ndani ya chumba
Endelea
Milio
ya risasi ikaendelea kurindima nje ya chumba tulichopo na kuzidi
kutupagawisha sote tuliopo ndani ya chumb hichi, wasiwasi mwingi ukawa
kwa dorecy ambaye fika anaoenekana kuchanganyikiwa
“eddy hao ni watu wa mume wangu”
Dorecy
alizungumza huku mwili mzima ukimtetemeka, nikapiga hatua za haraka
hadi dirishani na kuchungulia chini ambapo kuna umbali wa ghorofa mbili
kwenda chini.
“hatuwezi kutoka humu ndani”
Nilizungumza huku nikiwatazama dorery na phidaya
“itakuwaje sasa?”
Phidaya
alizungumza huku machozi yakimwagika kwa wingi.Nikapiga hatua hadi
mlangoni, nikachungulia kwenye sehemu ya kuingizia funguo, nikamshuhudia
jamaa mmoja akitandika risasi ya kichwa mzee mmoja aliye ambiwa alale
chini ila akaleta kiherehe cha kujinyanyua, ndipo akakutana na maafa
hayo ambayo ni yakinyama sana.
Gafla
simu ya phidaya ikaita na kutufanya sote kumgeukia na kumtazama kwa
macho ya mshangao, kwa kiwewe alicho nacho akashindwa hata kuikata na
kujikuta akiiachia na kuanguka chini, nikachungulia tena kwenye tobo la
kuingizia funguo na kumuona jamaa aliye muua mzee, akiutazama mlango
wetu kwa umakini.
“ingieni bafuni”
Nilizungumza
kwa sauti ya chinichini, dorecy akamshika mkono phidaya na kukimbilia
kwenye bafu liilopo humu ndani ya chumba changu.Jamaa akapiga hatua hadi
ulipo mlango uku bunduki yake aina ya ‘short gun’ ikiwa mkononi mwake.
Nikajibanza
nyuma ya mlango, huku mapigo ya moyo yakinienda mbio kiasi kwani bado
sijaiamini afya yangu kwa kiasi kikubwa kutokana na majeraha ya risasi
yaliyopo mwilini mwangu.Mlango taratibu ukafunguliwa, nikaanza kuona
kiatu cheusi kikitangulia mbele, jamaa akasimama kwa muda, gafla simu ya
phidaya iliyo anguka chini ikaanza kuita tena na kumfanya jamaa kupiga
hatua za taratibu hadi sehemu ilipo anguka simu na kuiokota.Mapigo ya
moyo yakazidi kunienda mbio, kwani endapo jamaa atageuka nyuma nilazima
ataniona.Akaitazama simu ya phidaya kwa muda na kuitupa chini na
kuchanguka, akatazama mlango wa kuingilia bafuni ambapo ndani yake yupo
phidaya na dorecy
Simu
ya jamaa ikaita, akaitoa kwenye koti lake, akaipokea nakuiweka sikioni
mwake, akazungumza kwa lugha ya kiarabu, nikastukia kumuona jamaa
akichomoka kwa kasi, ndani ya chumba pasipo kuniona nyuma ya mlango,
ving’ora vya gari za polisi, nikaanza kuvisikia na kunifanya nishushe
pumzi nyingi, na kujikalia chini, huku jasho jingi likimwagika.Ndani ya
dakika kadaa askari kadhaa wakawa wameingia katika sehemu tulipo, dorecy
na phidaya wakatoka bafuni, askari na madaktari walio salimika katika
vamizi la majambazi hawa
***
Wagonjwa
tulio salimika tukahamishwa kwenye hospitali moja, inayo milikiwa na
jeshi la nchi ya philipines, matiibabu yangu hayakuchukua muda mrefu
sana, nikaruhusiwa kutoka hospitalini na kuhamia kwenye hoteli ambayo
phidaya anaishi kwa siri sana, na amelipiwa gharama zote na dorecy
ambaye tayari amerudi kwa mume wake.
“phidaya,itatubidi turudi tanzania”
Nilizungumza
huku macho yangu yakimtazama phidaya aliye jilalia kiuvivu kwenye
kitanda, huku akiwa tumbo wazi akilichezea chezea kwa kiganja chake
tumbo lake lenye kiumbe ndani
“si usubiri niweze kujifungua kwanza”
“hatuwezi kuishi hapa, pasipo sisi kuwa na kazi, unadhani tutayamudu vipi haya maisha?”
“sawa mume wangu, je tukirudi huko tanzania, tutafikia wapi wakati umesha sema kwamba mama yako alitekwa na baba yako mkubwa”
Nikamtazama
phidaya kwa muda, kwani kitu alicho kizungumza kinamaana kubwa sana
kwangu, isitoshe sijajua ni hali gani inayo endela kati ya mzee godwin
na mama yangu.Nikanyanyuka taratibu na kuisogelea computer iliyopo
kwenye meza humu chumbani kwetu, ambayo imeunganishwa na huduma ya
internet.Nikaiwasha taratibu, baada ya muda nikafungua mtandao wa google
“unataka kufanya nini?” phidaya alizungumza huku akipiga hatua na kuja kukaa kwenye kiti nilicho kikalia mimi
“kuna mtu nataka kumtafuta”
“nani?”
“baba yangu mzazi, anaishi afrika kusini”
“mmmm sawa”
ENDELEA NAYO KUPITIA UBUYUBLOG.COM