Kurasa

Jumapili, 11 Septemba 2016

Tanesco Morogoro yaingia mzigoni kuwasaka wanaohujumu shirika hilo.



Shirika la ugavi wa umeme tanzania (TANESCO) mkoa wa Morogoro limeazisha operesheni kali ya kuwasaka na kuwakamata  watu wanaojihusisha na vitendo vya kuhujumu miundombinu ya shuirika hilo pamoja na wale wanaojiunganishia umeme kinyume cha sheria.

Ni operesheni kali ya kusaka na kuwakamata wezi wa umeme iliyofanyika majira ya usiku kwa kuhusisha maafisa wa Tanesco pamoja na jeshi la polisi katika maeneo mbalimbali ya manispaa ya Morogoro.

Operesheni hiyo imekuja kufuatia  watu wasiofahamika kuhujumu mali za shirika hilo katika maeneo tofauti ya manispaa ya Morogoro huku baadhi ya  wateja wakijiunganishia umeme kinyume na utaratibu hali iliyolazimu shirika hilo kufanya jitihada mbadala ili kunusuru miundombinu  na fedha za serikali zinazopotea kutokana na watu kujiunganishia umeme bila malipo.

Akizungumza wakati wa operesheni hiyo afisa usalama wa Tanesco mkoa wa Morogoro Chales Ngwila amesema katika oeperesheni hiyo wamefanikiwa kukamata watu wanaotuhumiwa kuhusika na tuhuma za kujiunganishia umeme kinyemela na kwamba zoezi hilo ni endelevu ili kukomesha matukio hayo.
chanzo; muungwana.co.tz

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni