christiano Ronaldo
Mshambuliaji tegemeo wa timu ya soka ya Real Madrid, Christiano Ronaldo usiku wa kuamkia leo kavunja rekodi ya mkongwe Alexandro Del Piero, kufuatia goli la faulo alilofunga usiku wa kuamkia leo.
Ronaldo anakuwa kafunga jumla ya magoli 12 ya faulo katika michuano ya UEFA na kuvunja rekodi ya Del Piero aliyekuwa kafunga goli 11 kwa faulo.
Alivunja rekodi hiyo kwenye mchezo kati ya timu yake na timu yake ya zamani iliyomlea tangu utotoni klabu ya Sporting CP ya nchini Ureno. Mtanange huo ulipigwa kwenye dimba la Santiago Bernabeu.
Sporting CP ni klabu ilimyolea Cristiano Ronaldo kutokea academy yao, hata hivyo hiyo haikuwa mechi rahisi kwa Real Madrid japo walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1 ila walilazimika kusubiri hadi dakika ya 90 kujihakikishia ushindi huo kupitia goli la kichwa la Alvaro Morata ikiwa ni dakika moja imepita toka Ronaldo asawazishe goli.
Goli la Sporting CP lilifungwa dakika ya 47 na Bruno Cesar.
Matokeo mengine tazama jedwali hapo chini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni