
Mapigano mapya yameanza kuhusu mzozo wa umiliki wa baadhi ya visima vikubwa vya mafuta katika maeneo ya Mashariki nchini Libya.
Afisa
mmoja wa usalama amekanusha kuwa vikosi vinavyomtii jenerali Khalifa
Haftar vinadhibiti miji ya Sirda, Ras Lanuf na Zuitina. Generali Haftar amekataa kutambua serikali ya umoja inayotambulika kimataifa huko Tripoli na kubaki upande wa watawala mahasimu wa Mashariki.
Chanzo; bbcswahili,com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni