![]() | |
Mgombea wa chama cha Democratic
nchini Marekani Bi Hillary Clinton amesema hakuficha taarifa za kuugua
homa ya mapafu kwa kuwa hakudhani kama litakuwa jambo kubwa na la
kusumbua.
Amekuwa akikosolewa kwa kushindwa kutoa taarifa zake
mapema mpaka pale alipokaribia kuanguka mbele ya hadhara katika siku ya
kumbukumbu ya shambulizi la Septemba 11.Akihojiwa na shirika la habari la CNN, Bi Clinton amesema kuwa hakufuata vyema kile anachokiita ushauri wa madaktari wake wa kupumzika kwa siku tano baada ya kufanyiwa vipimo siku ya Ijumaa. Timu yake ya kampeni imesema kuwa hana tatizo lolote la kiafya isipokuwa homa ya mapafu na kuongeza kuwa taarifa zaidi juu ya uimara wa afya yake zitatolewa. Trump amesema kuwa ofisi yake itatoa taarifa yake ya kiafya wiki hii. Bi Clinton alionekana kudhoofu kiafya siku ya kukumbukumbu ya watu waliofariki katika shambulio la Septemba 11,ambapo aliondoka katika eneo hilo kwa msaada maalum wa walinzi wake. Chanzo: bbcswahili.com |
Tanzania Entertainment News,Politics News ,Celebrity religion and Live Updates
Jumanne, 13 Septemba 2016
Hillary Clinton:Sina tatizo kubwa la kiafya
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni